Nini kinatokea nikipiga simu SACHA kwa huduma ya masaa 24?

Standard

Mutli Language Service 4Most folks don’t know that SACHA’s 24 Hour Support Line is available in over 300 languages.

To help spread the word, we’re posting information on what happens when you call in a few languages over the next few weeks.

Swahili, also known as Kiswahili, is a Bantu language and the first language of the Swahili people. Around five to fifteen million people speak Swahili as their first language; it is also used as a common language between speakers whose native languages are different in much of Southeast Africa, including Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Mozambique and the Democratic Republic of the Congo.

Jinsi yakupiga simu…

 • Kama unaweza tafuta eneo ukiwa peke yako kupigia simu.
 • Piga 905-525-4162.
 • Mwongozaji wa simu atapokea nakusema.”Karibu SACHA kituo cha msaada kwa wanaonyanyaswa kimapenzi.” Huyu sio mwajiriwa wa SACHA. Wapo pale kukuunganisha na mwajiriwa wa huduma za SACHA, na watakuuliza jina na namba yako ya simu.
 • Wakati mwongozaji atakapokuuliza jina unaweza mtajia jina lako la kwanza. Au jingine. Kama ni wewe tu ndio lazima upokee simu unaweza usipokee wakati mwingine.
 • Kama mwongozaji atakuuliza namba yako ya simu unaweza mpatia namba iliupigiwe simu na mtoa huduma wakujitolea, au kama huhitaji mkalimani, unaweza kusema huhitaji. Kama unahitaji mkalimani na huhitaji kutoa namba yako ya simu, tafadhali piga ofisi za SACHA kupitia nambari 905-525-4573, kati ya saa 3 asubuhi hadi saa 11 jioni kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa.
 • Endapo simu yako imefungwa, tafadhali mwambie mwongozaji wa simu kuhusu hilo.
 • Mtoa huduma wa kujitolea mwenye ujuzi wa SACHA atakupigia simu ndani ya dakika kumi au mara tu amalizapo kupokea simu zake za awali. Atajitambulisha kwa jina lake la kwanza nakukufahamisha kuwa anatokea SACHA. Atajitolea kukueleza kuhusu sera zetu za usiri.

Nini cha kuongelea

 • Unaweza ongelea chochote kuhusu kushambuliwa, kuhujumiwa, na kusumbuliwa kimapenzi.
 • Unaweza ongelea ni jinsi gani ukatili wa kijinsia ulivyo athiri maisha yako.
 • Unaweza ongelea jinsi ambavyo umekabiliana, na uzoefu wako kuhusu ukatili wa kijinsia au changamoto mpya za kukabiliana na hali hiyo ukijadiliana na mshauri wako wa wakujitolea.
 • Unaweza kuongelea kuhusu ridhaa, mipaka, imani potofu na uongo ambao tunafundishwa kuhusu shambulio la kimapenzi.
 • Unaweza ongelea jinsi ya kumsaidia rafiki au ndugu wa familia ambae ameshambuliwa kijinsia.
 • Unaweza ongelea kuhusu msaada ndani ya jamii kwa walionusurika.
 • Kama umewahi kushambuliwa, kusumbuliwa ama kuhujumiwa kimapenzi, utaamua ni kwa kiasi gani uelezee – kutokuongelea kabisa baadhi tu ya vitu/maelezo, ama zaidi.
 • Unaweza kuongelea kutoa taarifa polisi ama kwenda hospitali ukitaka.
 • Unaweza piga simu kama unahisi kuwa huenda kuna kitu kibaya kilichotokea.
 • Unaweza kuongelea kitu ambacho kimetokea au kitu cha zamani hata utotoni.
 • Unaweza ongelea kitu ambacho umesikia au umekisoma ambacho kinakukasirisha.
 • Unaweza ongelea kuhusu njia nyingine za ukatili na uzoefu wako na vile namna inavyo husiana na ukatili wa kijinsia –ubaguzi wa rangi,vita,mateso,vurugu za kinyumbani,umaskini,kuwa mkimbizi,ubaguzi wa mapenzi ya jinsia moja,ubaguzi wa wanaojiweza,na njia nyinginezo za ukatili na uonevu.
 • Unaweza kuonyesha hisia zako tu -ongea, cheka, lia, hasira.
 • Mnaweza kuwa kimya ninyi nyote kama hicho ndicho unacho hitaji.
 • Ni muhimu kujua chochote ambacho unaongelea kitasikilizwa na kuaminiwa.

Kile ambacho mtoa huduma kwa wateja wakujitolea anaweza kufanya kupitia simu

 • Kukusikiliza na kukuamini.
 • Kukufahamisha kuwa hilo sio kosa lako.
 • Kujadiliana nawe namna ya kuzikabili changamoto za kimawazo za kusaidia kupita wakati mgumu.
 • Kukupa taarifa kuhusu haki zako.
 • Kujibu matakwa yako kwa njia ya kitaalamu kufuatana na uzoefu wako na njiaza kukabiliana nazo wakati na hata baada ya tukio.
 • Kukubaliana na kuheshimu mawazo yako.
 • Kukupa taarifa kuhusu hatua za kupata matibabu au msaada wa kisheria. Mtoa huduma wakujitolea anaweza kuongozana nawe hosipitalini ama/au kituo cha polisi kama ukipenda.
 • Kushauri njia za kupata msaada zaidi na kukupa rasilimali.
 • Kuweka usiri kwa ulichokisema, muulize mtoa huduma wa kujitolea kama unawasiwasi kuhusu usiri.

Mawasiliano ya simu na mkalimani

Huduma kwa mteja SACHA zinapatikana masaa 24 na kwa Lugha zaidi ya 300!

 • Kupata msaada mkalimani tafadhali piga namba hiyo hapo juu, na toa jina na namba yako ya simu. Mtoa huduma wakujitolea atakupigia simu akiwa na mkalimani jirani yake. Kama unahitaji mkalimani na hutaki kutoa namba yako ya simu, tafadhali tupigie ofisini simu namba905-525-4573, kati ya saa 3 asubuhi na saa 11 joini, Jumatatu hadi Ijumaa.
 • Mkalimani, kama mtoa huduma ya kujitolea, atakuwa ni mwanamke.
 • Mkalimani pia anatakiwa kutilia maanani kuweka usiri kwa kile utakachosema.
 • Kama unamfahamu mkalimani na haupo huru kujieleza, tafadhali mueleze mtoa huduma wakujitolea. Tutafurahi kukupatia mkalimani mwingine.
 • Tafadhali jaribu kuweka kituo kila baada ya sentensi mbili au tatu, ili mkalimani aweze kukumbuka ulichosema na kukitafsiri kwa ufasaha kwa mtoa huduma wakujitolea.
 • Mkalimani anatakiwa atafsiri sawia na ulichokisema wewe na mhudumu wakujitolea bila kupunguza au kuongeza. Kama unadhani kuna kutoelewana, tafadhali sema. Makosa hutokea, na unachohitaji wewe ni kueleweka.
Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s